Description
TanzMED – Afya Rahisi, Popote Ulipo
TanzMED ni jukwaa la kidijitali la afya linalounganisha madaktari, hospitali, maduka ya bidhaa za Afya na urembo, maabara, huduma za afya nyumbani, na zana za afya zinazotumia AI ndani ya programu moja salama.
TanzMED imeundwa kwa ajili ya Afrika Mashariki ili kufanya huduma bora za afya zipatikane kwa urahisi, gharama nafuu, na kwa wakati wowote.
Afya yako. Programu moja.
--> Ushauri wa Daktari Mtandaoni
Wasiliana na madaktari na wataalamu wa afya waliothibitishwa kupitia mazungumzo ya video za papo kwa hapo (Instant) au kwa miadi (Appointment). Pata ushauri wa kitaalamu, ufuatiliaji wa afya, na rufaa bila kwenda popote ulipo.
:::: Huduma za Afya Nyumbani ::::
Weka miadi ya wauguzi, madaktari, au walezi kwa huduma salama na za kitaalamu ukiwa nyumbani au ofisini, ikijumuisha ufuatiliaji wa afya na huduma za matibabu.
:::: Afya ya Akili ::::
Pata msaada wa afya ya akili kupitia mazungumzo ya siri na wataalamu. Tumia zana na huduma za usaidizi zinazolenga kuboresha ustawi wa kihisia na kisaikolojia.
:::: Tathmini ya Afya kwa Kutumia AI ::::
Eleza dalili zako na upate tathmini ya awali inayotumia teknolojia ya AI ili kukusaidia kuelewa hali yako na hatua inayofuata ya kuchukua.
:::: Afya ya Mama na Mtoto ::::
Fuatilia maendeleo ya ujauzito, ratiba za chanjo, ukuaji wa mtoto, na upate ushauri wa wataalamu wa afya ya mama na mtoto.
:::: Afya ya Mwanamke ::::
Dhibiti mzunguko wa hedhi, uzazi, na afya ya uzazi. Pata msaada na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ya wanawake kupitia programu.
:::: Jamii ya Afya (Kijiwe cha Afya) ::::
Uliza maswali ya afya, shiriki katika mijadala, fuatilia mada za wataalamu wa afya, na jifunze kutoka kwa jamii inayojali afya. Ushiriki wa faragha unapatikana pale inapohitajika.
:::: Dawa na Vipimo vya Maabara ::::
Agiza bidhaa za Afya mtandaoni, weka miadi ya vipimo vya maabara, na pata huduma kutoka kwa maduka ya dawa na maabara zilizo karibu nawe.
:::: Elimu na Makala za Afya ::::
Soma makala za afya zilizoandikwa na kuthibitishwa na wataalamu, zinazojadili magonjwa ya kawaida, kinga, mtindo bora wa maisha, na ustawi wa afya kwa ujumla.
:::: Miadi ya Hospitali na Wataalamu ::::
Pata urahisi wa kuweka miadi na hospitali, maabara, na madaktari bingwa kupitia programu ya TanzMED.
Imejengwa kwa Uaminifu na Usalama
TanzMED imeundwa kwa kuzingatia usalama wa taarifa binafsi, faragha, na urahisi wa matumizi. Programu inapatikana kwa Kiswahili na Kiingereza ili kuwafikia watumiaji wengi zaidi Afrika Mashariki.
:::: Kanusho la Kitabibu ::::
TanzMED haitoi utambuzi rasmi wa magonjwa na haichukui nafasi ya ushauri au huduma za kitaalamu kutoka kwa mtaalamu wa afya.
Kwa dharura za kiafya, tafadhali wasiliana na huduma za afya za karibu mara moja.
Nouveautés (v7.0.16)
This release improves the Mental Health Mood Tracking experience with:
- AI-powered mood summaries
- Kijiwe posts linked to mood tracking
- Video-guided mental health activities
- Dynamic recommendations based on mood analysis
- Personalized wellness activities based on emotional state
- Improved activity detail pages